JINA JIPYA TULILOPEWA

Published on 00-00-0000


JINA JIPYA TULILOPEWA
Ninyi ni nuru ya ulimwengu .Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima (mathayo 5:14)
Mungu akaiona nuru ya kuwa ni njema Mungu akatenga nuru na giza (Mwanzo 1:4)
Bwana yesu ndiye anatoa majina ametupa majina mengi sisi wana wa Mungu , kama nuru, chumvi , wanafunzi ,wafalme na mengine mengi tu na bado limebaki jina moja kwa kila mtu ambalo atapewa mtu peke yake na hakuna mtu mwingine atakayelijua siku ile tukifika Mbinguni (Ufunuo 2:17) ila leo nataka tuangalie juu ya jina hili ‘Nuru’ . Inawezekana mara nyingi unasoma maandiko haya lakini leo nataka nikushirikishe mafunuo mengine kuhusu nuru .
Ukiwa mwana wa Mungu wewe si mwanadamu wakawaida, unakuwa na kitu kinachokutofoutisha na wanadamu wakawaida , unakuwa na utukufu wa Mungu ambao hauonekani kwa macho ya nyama ila unaonekana kwa macho ya kiroho . Mungu akikufungua macho ukamuona mwana wa Mungu utaona Nuru imemzunguka kama mwanga ,Nuru hii ipo kwasababu ndani yake yupo Mungu yupo Roho mtakatifu, huo ni ufukufu wa Mungu ambao mwana wa Mungu anakuwa nao. Mapepo yanachomwa na nuru hii ndiyo maana ukikaa karibu na mtu mwenye mapepo yanaripuka kwakuwa ni viumbe vya kiroho vinaumizwa na nuru hii inayokuzunguka , Hii ndiyo maana utaona wachawi wakisema mikono ya walokole ina moto,. Nuru yako inavyozidi kuongezeka ndivyo giza linavyozidi kukukimbia . Mapepo yatakukimbia ,dhambi zitakukimbia maana dhambi ni roho, wachawi watakukimbia , kila mwovu ataogopa kukushirikisha uovu . Unakuwa Nuru inayoangaza gizani na giza linakimbia.
Ujumbe wetu leo ni kwamba tumtafute sana Mungu tuzidi kujazwa Roho mtakatifu ili Nuru yetu izidi kuangaza gizani , giza halikai na Nuru hata siku moja, kuna watu wanajaribu kufukuza giza wakati wao wenyewe wako kwenye giza haiwezekani jambo hilo. Wanajaribu kukemea pepo lakini wao wenyewe wana dhambi ndani, giza halifukuzwi na giza. Wanakemea nguvu za kichawi lakini wao wenyewe wana roho za chuki ,tamaa ,wivu ,umbea usengenyaji hapo hakuna mafanikio.Mungu amenifunulia kwamba ukitaka kuushinda ufalme wa giza lazima uwe Nuru kamili . Lazima Mungu aingie ndani yako akutawale kikamilifu , lazima umpe nafasi ya kutosha kukutawala.
Mungu anatupenda ahadi zake kwetu nikweli kabisa , Bwana wetu Yesu yupo wakati wote anataka akutie Nuru, yeye ndiye abatizaye kwa Roho mtakatifu mtafute sana akujaze zaidi uwe Nuru kamili. (Yohana 1:9) “kulikuwa Nuru halisi amtiaye nuru kila mtu,akija katika ulimwengu”.(Yohana 8:12) “basi Yesu akawaambia tena akasema ,mimi ndimi nuru ya ulimwengu yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe bali atakuwa na nuru ya uzima” Hata sasa Bwana Yesu yupo anataka tumuonyeshe nia yakutaka kuwa nuru kamili hakika ni muaminifu atatufanya kuwa na nuru ya uzima.
Usikubali kuwa Mkristo wa historia kuna watu husema kwamba; mimi zamani nilikuwa na nguvu za kiroho kweli, zamani nilikuwa naona maono zamani nikuwa nasikia sauti ya Roho Mtakatifu. Ukristo siyo mambo ya historia tunazaliwa na kukua mpaka kufikia utimilifu wa kristo hatuzaliwi na kufa . (Ufunuo wa Yohana 3:1) Na kwa malaika wa kanisa liliko sardi andika haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu na zile nyota saba .Nayajua matendo yako ,yakuwa unajina la kuwa hai ,nawe umekufa . Kuwa mkristo wa historia nikuwa na jina lakuwa hai lakini umekufa . Usikubali kuwa mkristo wa historia uamsho wa kanisa unaaza na wewe ,unaaza na mtu mmoja mmoja, mtu ni kanisa. Tumtafute Mungu kwa bidii tusije tukawa tunaitwa Nuru lakini kumbe tumekufa.

TUMEWEKWA HURU KWELI KWELI

Published on 00-00-0000


TUMEWEKWA HURU KWELI KWELI
Basi Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli [Yohana 8:36]. Atukuzwe Bwana Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi kwa Upendo wake waajabu wa kumtoa mwana wake wa pekee Yesu kristo ili afe msalabani na kutukomboa na kututoa katika vifungo vyote vya yule mwovu na kutufanya wana wa Mungu , wana wa Ufalme wa Mungu na warithi wa ahadi za Mungu. Wokovu aliotupa umetuweka huru mbali na kila tanzi na vifungo vya Shetani, hiyo ndiyo kazi iliyomleta Duniani . Je unaamini hilo ?
Nimeona wakristo wengi wanasema, tumeokoka lakini wanarudi nyuma kwasababu ya kumuogopa Shetani wanaishi kwa hofu ,wanaogopa Wachawi na Nguvu za giza wanajihisi bado wana laana na maagano ya mababu. Wanaitwa huku na huko kwenda kuombewa maombi ya kuvunja maagano wanaambiwa watoe sadaka za kuvunja maagano ya Mababu ,haya ni maajabu! mtu aliyeokoka anatoa wapi maagano ? wengine wanaenda kufanya maombi ya kuvunja Madhababu ,wanaambiwa zipo madhabahu za Mababu zinawafuatilia haya nayo ni maajabu! tena maombi hayo wanaambiwa wayaambatanishe na sadaka nono . Hakuna kitu kama hicho kwa mtu aliyeokoka ., sadaka ya wokovu ni Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, kila aliyeokoka amefunguliwa kutoka katika vifungo vyote vya dhambi na kila aina ya Maagano na Madhabahu za Shetani , najua kuna watu niwabishi kuhusu hili waendelee kubisha wafuasi wa Injili ya ukombozi, lakini ukweli ni kwamba kuokoka sio kujiunga na madhehebu ya kipentekoste kuokoka ni kuzaliwa mara ya pili kwa Roho mtakatifu, Roho mtakatifu ni Mungu ,Mungu hakai kwenye hekalu linalomilikiwa na maagano ya Shetani na laana , kama kuna mtu bado hajafunguliwa katika vifungo vya Shetani bado hajaokoka anatakiwa aendelee kuomba toba ya dhati na kumtafuta Mungu kwa bidii mpaka abatizwe ubatizo wa Roho mtakatifu na Bwana Yesu mwenyewe. Tumewekwa huru kweli kweli.
Vifungo vya Shetani vitaondoka kwa mtu, kama yeye mwenyewe atakata shauri na kukubari kuomba toba ya dhati kabisa na kumpokea Bwana Yesu kuwa ni Mwokozi wake milele, ndipo atafunguliwa na kubatizwa kwa Roho , kufunguliwa kwa mtu hakutegemeani na Nguvu za kiroho za mtu anayeombea ila inategemeana na toba ya mtu anayeombewa, utayari wake wakuishi na Mungu ,utayari wake wakuishi maisha matakatifu. Waambieni watu ukweli, kama mtu anataka kuwa huru inampasa aokoke, hakuna njia ya mkato kwa Mungu.
Angalia Bwana anavyosema mwenyewe katika Isaya “Roho ya Bwana Mungu i juu yangu kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo kuwatangazia mateka uhuru wao na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao” [Isaya 61:1] .Hii ndiyo kazi iliyomleta Bwana wetu Yesu kutuweka huru kutufungua kutoka katika vifungo vya yule mwovu .Unabii huo ulitolewa na nabii Isaya siku nyingi kabla ya kuja kwa Bwana Yesu Duniani , Bwana Yesu mwenyewe kasoma unabii huo na kusema maneno hayo yametimia “Roho wa Bwana yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao ,na vipofu kupata kuona tena kuwaacha huru waliosetwa .Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi ,akaketi, na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho .Akaanza kuwaambi leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu” [Luka 4:18-21]. Maandiko hayo yametimizwa, kazi iliyomleta aliimaliza msalabani sadaka ya wokovu imekwisha tolewa tupo huru kweli kweli. Hatuna haja ya kuwa na hofu na kazi zote za Shetani .
Mbinu ya shetani anayoitumia moja wapo ni kuwatia hofu watu wa Mungu ili wakose Imani kwa Mungu wao na kujaribu kujitetea wenyewe . Angalia Shetani alivyoingia ndani ya Petro ili amtie Hofu Bwana Yesu “Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu ,na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani na waandishi na kuuwawa na siku ya tatu kufufuka Petro akamchukua akaanza kumkemea akisema ,Hasha Bwana hayo hayatakupata .Akageuka akamwambia Petro ,Nenda nyuma yangu Shetani u kikwazo kwangu maana huyawazi yaliyo ya Mungu bali ya wanadamu”. [Mathoyo 16:21-23]. Shetani alitaka amtie hofu Bwana Yesu .Na hata leo ndicho anacho fanya kuwatia watu hofu. Watu wanaogopa freemason hawajui kwamba ni wachawi wakawaida tu. ,wakinunua ngua wanaazaa kuuliza -uliza hizi zimetengenezwa wapi? Zina alama za freemason au hazina ? wanaogopa na vipodozi wanauliza hivi mbona kama vina alama za freemasoni ? huu ni ujinga ni kutojitambua kwamba wewe ni mwana wa Mungu. Usiogope nguvu za giza hazina mamlaka kwako. Mtume Paulo aliwahi kuwaonya watu juu ya jambo hili “Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni ,bila kuuliza –uliza ,kwa ajili ya dhamiri” [1Wakorintho10:25]. Tumepewa mamlaka ya kuvunja na kung’oa kila pando la Shetani katika kila tulicho nacho. Mungu pia ni mwaminifu mwenye Rehema na Upendo wa ajabu ahadi zake ni kweli anasema “ Malaika wa BWANA hufanya kituo akiwazungukia wamchao na kuwaokoa” [Zaburi 34:7] Angalia jinsi alivyomlinda Ayubu “Ndipo Shetani akamjibu BWANA na kusema je? Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure?wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote pamoja na nyumba yake na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibariki nayo mali yake imeongezeka katika nchi”[Ayubu1:9-10] . Hivyo ndivyo Shetani anavyokuona mwana wa Mungu usiogope, wala usihofu Nguvu za giza ,ukiokoka huna laana wala huna maagano uko huru kabisa anayekuambia unalaana au unamaagano anakutia hofu ukose Imani na wokovu wako ,.”Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini ;Ninyi mkikaa katika neno langu mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru”[Yohana 8:31-32]
Lakini leo hii utashangaa mtumishi anajiita mtumishi wa Mungu anaenda kanisani kufundisha kuvunja maagano ,tena kanisa la watu wanaojiita wameokoka ,anawaambia leteni sadaka za ukombozi na wakristo na wachungaji wao wanaunga mkono .Fukuzeni hao Mungu amenionyesha kwamba ni majambazi ,ni wezi wanawaibia watakatifu ambao bado hawajukua vizuri kiroho, wanawatia hofu wamuogope Shetani, badala ya kumtukuza Mungu anayewalinda wakati wote.

MAOMBI YANADHIHILISHA IMANI YAKO KWA MUNGU

Published on 00-00-0000


MAOMBI YANADHIHILISHA IMANI YAKO KWA MUNGU
Mungu anapenda aone jinsi unavyomtegemea yeye. Imani ni kuwa na uhakika, Je unaonyeshaje uhakika wako kwa Mungu? Mungu anataka umuonyeshe kwamba unamtegemea yeye katika kila jambo na unamuamini yeye tu, kwamba ndiye anaweza kuyafanya yote na huna msaada mwingine zaidi yake. Maombi yanadhihiliha imani hiyo.
Angalia mfano huu:- “Aliposikia kwamba ni Yesu wa Nazareti aliyekuwa anapita mahali hapo, alianza kupaza sauti, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!” Watu wengi walimkemea ili anyamaze, lakini yeye akazidi kupaza sauti, “Mwana wa Daudi, nihurumie!” Yesu alisimama, akasema, “Mwiteni.” Basi, wakamwita huyo kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo! Simama, anakuita.” Naye akatupilia mbali vazi lake, akaruka juu, akamwendea Yesu.Yesu akamwuliza, “Unataka nikufanyie nini?” Huyo kipofu akamwambia, “Mwalimu, naomba nipate kuona.” Yesu akamwambia, “Nenda, imani yako imekuponya.” Mara huyo kipofu akaweza kuona, akamfuata Yesu njiani.” (Marko 10: 47-52)” , Bwana Yesu alimuambia mtu huyu kwamba imani yako imekuponya , sasa tunaona jinsi mtu huyu alivyodhihilisha imani yake ,alidhihilisha imani yake kwa Bwana Yesu kwa kuzidi kuomba hata alipokatishwa tamaa bado hakukubari alizidi tu kuomba alizidi kupaza sauti ,hivyo ndivyo alivyodhihilisha imani yake kwa Mungu .Kazana kuomba udhihilishe imani yako kwa Mungu Paza sauti yako kwa Mungu wako udhihilishe Imani yako kwa Mungu wako, hata kama bado huoni majibu yoyote ,Mbingu bado zimefunga kwako wewe endelea kupaza sauti yako tu. Utafika wakati Bwana Yesu atasema Imani yako imekuokoa.
Angalia mfano huu tena “na tazama ,mwanamke mkananayo wa mipaka ile akatokea akampazia sauti akisema ,unirehemu Bwana mwana wa Daudi ,binti yangu amepagawa sana na pepo wala yeye hakumjibu neno .Nao wanafunzi wake wakamwendea wakamwomba ,wakisema mwache aende zake kwa maana anapiga kelele nyuma yetu, Akajibu ,akasema sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli , Naye akaja akamsujudia akisema Bwana unisaidie .Akajibu akasema si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa ,Akasema ndiyo Bwana lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao .Ndipo Yesu akaji akamwambia ,mama Imani yako ni kubwa na iwe kwako kama utakavyo .Akapona binti yake tangu saa ile” .(Mathayo 15:22-28)
Angalia jinsi gani bwana Yesu alivyoona Imani ya huyu mama, ni mambo gani huyu mama aliyafanya mpaka Bwana Yesu akasema mama Imani yako ni kubwa. Aliomba sana hata aliponyamazishwa hakukubali alizidi kuomba bidii yako ya kuomba inazidi kudhihilisha Imani yako kwa Mungu . kuomba kunadhihilisha Imani yako mpendwa, kazana kuomba. “Hatimaye Bwana Yesu atasema Imani yako ni kubwa na iwe kwako kama utakavyo”.
Angalia mfano huu mwingine “Nawalipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano waliitoboa dari pale alipokuwapo na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza Naye Yesu alipoioona Imani yao akamwambia yule mwenye kupooza mwanangu ,ummesamehewa dhambi zako” (marko 2:4-5). Hawa watu walihangaika sana wamfikishe mgonjwa wao kwa Bwana Yesu lakini watu walikuwa wengi wakishindwa kumfikia Bwana Yesu hatimaye wakaamua kubomoa dari Bwana Yesu aliyoona Imani yao kwa jinsi walivyohangaika kumfikia .
Unavyohangaika kumtafuta Mungu na kumuomba ndivyo unavyodhihilisha Imani yako kwake kwamba yeye pekee ndiye anaweza kukuokoa katika hilo jambo na hapo ndipo unapo pokea muujiza wako. Usihangaike kutafuta watu wewe mtafute Mungu ,usimpazie sauti mtu wewe mpazie sauti Mungu , anaweza kuyafanya mambo yote. Kuna watu wakipata matatizo wao huhangaika zaidi kutafuta watu lakini Mungu anataka tuhangaike kumtafuta yeye, ndivyo unavyodhihilisha Imani yako kwake . Hatimaye atasema imani yako imekuokoa .”Onyesha Imani yako kwa Bwana Yesu kwa kuhangaika kumtafuta”

MAOMBI YANAONGEZA UHUSIANO WAKO NA MUNGU

Published on 00-00-0000


MAOMBI YANAONGEZA UHUSIANO WAKO NA MUNGU
Hakuna watu wawili ambao wanaweza kushirikiana pasipo kuongea ,haiwezekani kabisa kuwa na mahusiano pasopo kuwasiliana,vile vile mawasiliano ya watu wawili yanapopungua ndivyo mahusiano yao yanavyokufa .Jambo hili halina tofauti na upande wa Mungu wetu na watoto wake, kila wakati Mungu wetu anapenda kuwasikia watoto wake .Lakini Je watoto wake wako tayari kusema na Baba yao? .Je tuko tayari kusema na Mungu Baba yetu kama yeye alivyotayari kutusikiliza? Anasema hivi “Haya leteni maneno yenu asema Bwana toeni hoja zenu zenye Nguvu asema mfalme wa yakobo” [Isaya 41:21]. Pia anasema “Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu ombeni mtakalo lolote nanyi mtatendewa” [Yohana 15:7] “Nami nawaambia ,ombeni nanyi mtapewa tafuteni nanyi mtafunguliwa” [ Luka 11:9] “ Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki na masikio yake hukielekea kilio chao [ Zaburi 34:15] .Hivyo ndivyo BWANA Mungu wetu anavyosema anapenda kusikia kutoka kwetu ameweka mlango ulio wazi kwa kila mtu kusema naye. Pazia la Hekalu limepasuka linampa kila mtu fulsa yakuingia na kusema na Mungu. Tuna karibishwa na tuna haki ya kuongea na Mungu wetu Je uko tayari kusema na Baba kama yeye alivyotayari kukusikiliza ?
Ukisema na Mungu kila wakati unaongeza mahusiano yako na yeye hivyo basi unazidi kushikamana naye katika njia zako. Ukipunguza kuomba ndivyo unavyozidi kupunguza mahusiano yako na Mungu , na ndiyo unavyo muacha Mungu na ndivyo unavyozidi kufa kiroho , Mungu hamuachi mtu lakini mtu ndiye anamuacha Mungu ,na njia moja wapo anayoitumia Shetani kuwafanya watu wamuache Mungu nikuwazuia kuomba, kuwazuia kuzungumza na Baba yao.
Ukristo siyo Imani ya kuombewa ombewa ni Imani ambayo kila mtu anatakiwa kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na Mungu wake , Hii haina maana hatuombeani lakini kila mtu ana haki yakuongea na Mungu Baba .Unapokuwa mtu wa kusema na Mungu na yeye pia atakujulisha juu ya mambo mbali mbali , atakujulisha juu ya maisha yako ,huduma yako kanisa lako na hata hatari inayotaka kukupata .Anasema hivi “Hakika BWANA Mungu hatafanya neno lolote ,bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake” [Amosi 2:7] .Ni ukweli kwamba kila aliyejazwa Roho mtakatifu anasema na Mungu kupitia maono ,ndoto ,njozi na kutumiwa malaika, hivyo basi mambo haya yanatokea kwa wale ambao wanasema na Mungu . Mungu anasema na wanao sema naye ,anawapa siri wale wanaosema naye.
SEMA NA MUNGU KILA WAKATI ILI ASEME NA WEWE KILA WAKATI

USIMUEKEE MUNGU MIPAKA

Published on 07-03-2020


USIMUEKEE MUNGU MIPAKA
Mwana wa Mungu leo nataka tuone Jambo moja kuhusu kuomba unapomuomba Mungu usimuekee mipaka ya utendaji . Baba Mungu mwenyenzi muumba wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana hana mipaka ya utendaji , wala njia zake za kutenda kazi hazichunguziki na ziko nje ya uwezo wa fikra za mwanadamu ndiye mwenye mamlaka ya kila kitu. “Tazama ,mimi ni BWANA ,Mungu wa wote wenye mwili ;je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?” (Yeremia 32:27)
Katika kuomba wapo watu ambao wanampangia Mungu jinsi ya kuleta majibu ,wakiona maombi yao hayajibiwi kama wanavyotegemea basi hukata tamaa nakuona hilo jambo haliwezekani tena , angalia mfano huu ambao tunaupata katika Biblia:-
“ Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha ukuhani cha Abiya. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni. Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama. Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana. Siku moja, ilipokuwa zamu yake kutoa huduma ya ukuhani mbele ya Mungu, Zakaria alichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwa desturi, kuingia hekaluni ili afukize ubani. Watu, umati mkubwa, walikuwa wamekusanyika nje wanasali wakati huo wa kufukiza ubani. Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani. Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. Lakini malaika akamwambia, “Zakaria, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.
Utakuwa na furaha kubwa na watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake. Atakuwa mkubwa mbele ya Bwana. Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake. Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao. Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama ya Elia. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake.” Zakaria akamwambia huyo malaika, “Ni kitu gani kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi ni mzee, hali kadhalika na mke wangu.” Malaika akamjibu, “Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele ya Mungu; nimetumwa niseme nawe, nikuletee hizi habari njema. Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambia yatakapotimia.”( Luka 1:5-20)
Zakaria Kuhani ambaye anamfahamu Mungu vizuri, alimuomba Mungu kwa muda mrefu apate mtoto, lakini mke wake alipokuwa mzee aliacha kuomba kwasababu aliamini hawezi tena kupata mtoto , kwasababu akili zake za kibinadamu zilifika mwisho akaona hata uwezo wa Mungu nao umefika mwisho, kumbe Mungu hana mipaka ya utendaji kazi . Zakaria anamhoji malaika itawezekanaje jambo hili ikiwa mke wangu ni mzee? Matokeo yake Mungu akampa adhabu ya kuwa bubu kwakuwa hakuamini uweza wa Mungu katika utendaji, Mungu wetu hana mipaka ya utendaji kama mwanadamu.
Ukimuomba amini kwamba jambo unaloomba atajibu kwa njia yoyote ile sio lazima hiyo unayowaza wewe. Ana njia nyinyi za utendaji uweza wake hauchunguziki. Unaweza kumuomba Mungu akupe kazi uliyosomea lakini si lazima akupe hiyo, anaweza kuleta nyingine au akainua njia nyingine za uchumi .Kumuekea Mungu mipaka kutakufanya ukate tamaa katika kumuomba kwasababu pale utakapoona akili zako zimefika mwisho unafikiri na uweza wa Mungu umefika mwisho.
Bwana Yesu asifiwe !
Mungu awabariki.

Mungu wetu ni Mungu aliye karibu

Published on 06-03-2020


‘’Mimi ni Mungu aliye karibu asema BWANA, Mimi si Mungu aliye mbali’’ (Yeremia 23:23 .Mungu wetu yuko karibu si Mungu aliye mbali, yupo na sisi anakaa ndani yetu, “nami nitatia roho yangu ndani yenu ,na kuwaendesha katika sheria zangu ,nanyi mtazishika hukumu zangu ,nakuzitenda (Ezekiel 36:27) Mungu wetu anaishi pamoja na sisi, hii ndiyo maana ya jina la Bwana wetu Yesu kristo [Imanueli] yaani Mungu pamoja na wanadamu ,na ameahidi kwamba hatatuacha mpaka ukamilifu wa dahari. [Mathayo 28:20]
Hii inamaana gani kujua kwamba Mungu yuko karibu? Hii inamaana kwamba tuwe na imani katika kuomba tuamini kwamba Mungu anasikia maombi yetu, tuamini kwamba Mungu anaona kila jambo letu, Mungu anaona kila teso letu, Mungu anawaona Maadui zetu, Mungu anajua hali zetu hivyo basi tunapoomba tusiwe na hofu tuwe na uhakika. Hii inamaana gani tena ? Hii inamaana kwamba tuzidi kuishi maisha matakatifu kwa kuzidi kujiepusha na kila uchafu wa hii Dunia , maana Mungu aliye Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu hakai kwenye Hekalu chafu.Online Visitors Counter